[Intro]
Eti-lah-lah-lah, lalalala, lala, lalaah
Lah-lah, lalalala, lala, lalaah
[Verse 1]
Nna hamu mwenzenu nna hamu kuyahadithia
Oh nna hamu tena nna hamu kuyasimulia
Utani kama utani tulianza kimasiara
Sikudhani sikudhani yatafikia mahala
Akiwa hapatikani hapaliki sijalala
Kanifanya kitu gani? Mbona imekua mara?
Dua la kuku menipata mwewe wallah nyinyi ni mtihani
Hata makosa ayafanye yeye mimi ndo naomba samahani
[Pre-Chorus]
Ona anacheka kama mazuri
Anajua kabisa amenteka kwake sina shughuli
Eti kumwacha naanzaje sa kusepa natoa wapi jeuri
Na kwenye koma kaeka nukta kanitia na kufuli
[Chorus]
Oh, baby mimi hapa taabani (Wewe utaniuwa niuwa)
Nimeoza dah yarabi sihemii ( Wewe utaniuwa niuwa)
Ah, izo raha zakoo (Wewe utaniuwa niuwa)
Roho yangu mali yako (Wewe utaniuwa niuwa)
[Verse 2]
Tukikosa stuli ni sunna kula kwenye mkeka
Unijue vizuri nikinuna mie ndo nadeka
Husijedhani kiburi uniache nikaja kuchekwa
Baby raha ya shughuli mkunwa awe na heka heka
Oh husichokipenda wewe chunga na mimi husinifanyie
Mgomba wangu mwenyewe eti ndizi nigombanie
Nipe penzi nilewe umenizimiaa
Ooh ringa kwangu upo mwenyewe kiboko yangu miee, oh vimbaa
[Pre-Chorus]
Ona anacheka kama mazuri
Si anajua kabisa amenteka kwake sina shughuli
Eti kumwacha naanzaje sa kusepa natoa wapi jeuri
Na kwenye koma kaweka nukta kanitia na kufuriii
[Chorus]
Oh, baby mwenzako mimi twabani (Wewe utaniuwa niuwa)
Chagua mwenyewe unizike unishafirishe (Wewe utaniuwa niuwa)
Ah, izo raha zakoo (Wewe utaniuwa niuwa)
Roho yangu mali yako oh (Wewe utaniuwa niuwa)